Vyakula vya kutumia kabla ya kunywa pombe

Unachokulaa kabla ya kunywa pombe kinaweza kuathiri sana
jinsi unavyohisi mwisho wa usiku-na asubuhi baada ya kuamka.

Kula chakula kablla ya kutumia kileo kunaweza kukusaidida
kudhibiti njaa, kusawazisha chumvi chumvi mwilini na kupunguza athari mbaya
zinazohusiana na pombe.

Kwa upande mwingine, kuchagua vyakula vingine kunaweza
kusababisha kupata gesi, ukosefu wa maji mwilini, kiungulia, na matatizo ya
kumeng’enya chakula.

Vyakula vyenye kiwango kikubwa cha protini kama vile nyama,
mayai, na samaki vinashauriwa kula kabla ya kunywa pombe. Vyakula hivi husaidia
kupunguza kasi ya kuchanganywa kwa pombe tumboni na hivyo kupunguza kasi ya
kunywa pombe. Pia, vyakula vyenye wanga kama vile mkate, viazi, na mchele pia
husaidia kupunguza kasi ya kunywa pombe. Inashauriwa kuepuka vyakula vyenye
kiwango kikubwa cha mafuta kama vile nyama zenye mafuta mengi, vyakula vya
kukaanga, na vyakula vyenye sukari nyingi, kwani hufanya mwili kuchukua muda
mrefu zaidi kuyeyusha na kuchakata vyakula hivyo na hivyo kuongeza hatari ya
kunywa pombe nyingi haraka. Ni muhimu kukumbuka kwamba kula chakula hakuna
dhamana kwamba hutapata ulevi wa pombe, hivyo ni muhimu kuzingatia kipimo
salama cha pombe na kutokunywa pombe na kuendesha gari.

Vifuatavyo ni aina ya
vyakula ambavyo unaweza kula kabla ya kunywa kileo/pombe

Mayai: Mayai yana
virutubisho na yana angalau gramu 6 za protini kwa kila yai.

Kutumia vyakula vyenye protini kama mayai kabla ya kunywa
pombe kunaweza kusaidia kupunguza muda wa chakula kuisha tumboni na
kuchelewesha pombe kunfyonzwa tumboni,

Pamoja na protini, mayai yana lishe bora zaidi ambayo
itakufanya kujihisi kushiba kwa muda mrefu na kupunguza njaa inayosababishwa na
pombe baada ya kuamka asubuhi.

Shayiri: Shayiri
ni chanzo kikubwa cha nyuzinyuzi chakula na protini, vyote hivi hukufanya
kujihisi umeshiba na kupunguza athari za pombe.

Nusu kikombe cha shayiri ambayo haijapikwa hutoa karibu 5g
ya protini na 4g ya nyuzi, pamoja na viwango vya wastani vya mahnesium,
selenium na chuma.

Mbali na lishe yake, uchunguzi mmoja wa zamani ulibaini
kwamba shayiri zinaweza kuboresha afya ya ini na kuboresha utendaji kazi wake. Tafiti
kwa wanyama zinaonyesha shayiri husaidia kukinga ini dhidi ya madhara
yatokanayo na pombe.

Ndizi: Ndizi
kubwa zinaangalau 4g za protini, kula ndizi kabla ya kunywa pombe kunasaidia
kuchelesha pombe kufyonzwa katika tumbo.

Ndizi zina potasiamu nyingi, na pia zinajumuisha karibu 75%
ya maji. Kunywa pombe hukufanya kukojoa sana, na kusababisha upungufu wa maji
mwilini na kupoteza chumvi. Maji pamoja na potasiamu kunasaidia kusawazisha
kiwango cha chumvi na maji mwilini baada ya kunywa pombe

Ndizi za njano (mbivu) pia zina nyuzinyuzi, ambazo hupunguza
unyonyaji wa pombe ili usilewe haraka sana. Na kwa wanywaji wenye vidonda vya
tumbo, ndizi husaidia kupambana na aside ya tumbo kukukinga na kiungulia na
usumbufu mwingine wa tumbo.

Mtindi wa Kigiriki
ulio na protini nyingi:
Mtindi ni chakula kingine maarufu cha kusaidia usagaji
chakula. Yoghurts nyingi zina bakteria rafiki mwilini ambao huitwa probiotics ,
ambayo inaweza kusaidia kuzuia kuhara na matatizo mengine yanayohusiana na
magonjwa ya tumbo.

Mtindi wa Kigiriki pia una protini nyingi, pamoja na mafuta
na wanga. Itakufanya ushibe kwa muda mrefu kwa sababu protini huyeyushwa polepole,
ambayo pia hupunguza kasi ya ufyonzwaji wa pombe mwilini mwako.

Tikiti maji: Tikiti maji ni vyema
kutumiwa kabla ya kunywa kwa sababu lina maji mengi, ambayo husaidia kuupa
mwili unyevu. Kula tikitimaji na vyakula vingine vya kuongeza maji kunaweza
kusaidia kuzuia upungufu wa maji mwilini unaohusishwa na unywaji pombe.

Salmon: Samoni ni samaki mkubwa
mwenye mnofu mwekundu. Samoni ana vitamini B12 kwa wingi, kirutubisho muhimu
ambacho mara nyingi hupungua kwa unywaji wa pombe. Pia ana
protini nyingi na mafuta yenye afya, ambayo yanaweza kupunguza ufyonzwaji wa pombe
mwilini. Ili kupata mlo bora wa kabla ya kunywa, choma samaki aina ya
samoni (kibua) na uiambatanishe na parachichi na nafaka nzima uzipendazo.

Maji: Pombe ni
diuretic (inakufanya ukojoe mara kwa mara).  Kwa sababu hii, kunywa bilauli chache za maji
ni mojawapo ya mambo muhimu zaidi unayoweza kufanya kabla ya kunywa. Mbali na
maji ya kunywa, unaweza pia kula vyakula vyenye maji mengi kama tango,
jordgubbar na lettuce.

Kuku: Kuku wana wingi wa
protini, kunaweza kusaidia kupunguza kasi ya pombe kufyonzwa mwilini. “Protini,
pamoja na mafuta na nyuzinyuzi, huchukua muda mrefu kusagwa hivyo inaweza
kusaidia kupunguza kasi ya jinsi kiwango cha pombe katika damu huongezeka”.

Parachichi: Parachichi lina
potasiamu, chumvi muhimu ambayo mara nyingi hupungua kwa unywaji wa pombe
kupita kiasi. Kwa kiasi fulani katika lishe, parachichi pia lina mafuta
mengi yenye afya, ambayo huyeyushwa polepole ili kushiba na inaweza kupunguza
unyonyaji wa pombe kwenye damu yako. Moja ya mambo bora kuhusu parachichi
ni kwamba unaweza kuiongeza kwa urahisi karibu na mlo wowote.

 

 

 

Latest

ERYKO (Erythromycin Stearate Tablets)

ERYKO (Erythromycin Stearate Tablets) is a medication that belongs to the macrolide antibiotic class, commonly used for the treatment of bacterial infections such as...

Is your parenting styles a better guide

<!-- Start_mdn_ads_blog_post_page --> 2023-11-06 Parenting styles Since childhood, you are the onlooker of your friend’s family where he was raised...

Teething in babies – Wellness

<!-- Start_mdn_ads_blog_post_page --> 2023-09-19 Teething in babies When your baby starts to grow, you will notice certain changes in his...

7 Surprising Ways Deadlifts Can Boost Your Health And Fitness Goals in 2023

Credit: PixabayAre you seeking exercise to help you achieve your health and fitness goals? Look no further than the deadlift! This full-body exercise targets...

Discover The 7 Mysterious Types of Nutrition and Why It’s Crucial

Unravel the mystery behind the seven types of nutrition. From Autotrophic Nutrition to Heterotrophic Nutrition, Holozoic Nutrition, Saprophytic Nutrition, Parasitic Nutrition, Symbiotic Nutrition, and...